Sat

07

Jun

2014

Uchaguzi Syria, ni tangazo la kufeli njama za maadui

Kiswahili

Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah nchini Lebanon, amesema kuwa, hatua ya wananchi wa Syria ya kushiriki kwa wingi katika uchaguzi wa rais wa nchi hiyo, umeuthibitishia ulimwengu kwamba, mashinikizo ya Wamarekani na madola ya Magharibi na Kiarabu dhidi ya Syria, yameshindwa. Aidha Sayyid Hassan Nasrullah amesema kuwa, uchaguzi huo ni tangazo la kisiasa na kitaifa la kufeli vita dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu. Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah nchini Lebanon ameyasema hayo katika maadhimisho ya kumuenzi Allamah Sheikh Mustwafaa Quswair, yaliyofanyika katika ukumbi wa Shahid Sayyid Muhammad Baqir Swadri katika shule ya Imam Mahdi AS mjini Bairut, Lebanon. Ameashiria vitisho vilivyotolewa kwa lengo la kuzuia uchaguzi wa rais nchini Syria na kusema kuwa, vitisho hivyo havikuwa na taathira yoyote, bali serikali ya Damascus ilisimama imara katika kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika katika tarehe iliyopangwa. Ameyahutubu, madola hayo ya Magharibi na waitifaki wao katika eneo la Mashariki ya Kati kwa kusema kuwa, yalitakiwa kuruhusu zoezi hilo kufanyika katika balozi za Syria ndani ya mataifa hayo ili waone kama ushiriki wa Wasyria ungekuwa mdogo au laa! Amesema Sayyid Hassan. Aidha amesema uchaguzi huo umedhihirisha ukweli huu kwamba, wananchi wa Syria ndio waamuzi na wenye kauli ya mwisho kuhusu mustakbali wa taifa lao na kwamba, vita vinavyoendelea nchini humo si kati ya serikali na wananchi, bali ni kati ya serikali na maadui wa taifa. Aidha amesema kuwa, ushiriki mkubwa wa wananchi umeonyesha kwamba raia wa nchi hiyo bado wana imani na serikali ya Rais Bashar al-Assad wa nchi hiyo. Amesema, yeyote anayetaka kutatuliwa mgogoro wa nchi hiyo kwa njia za kidiplomasia, hawezi kuupuuza uchaguzi wa rais nchini humo, hasa kwa kuzingatia kwamba uchaguzi huo umetoa ujumbe kwamba, utatuzi wa kisiasa wa mgogoro wa nchi hiyo, utaanza na kumalizika sambamba na Rais Bashar al-Assad kuwepo madarakani. Kwa upande mwingine amezungumzia propaganda zinazoenezwa na maadui kuhusiana na kadhia ya Lebanon na kusema kama ninavyomnukuu: "Wote mnapaswa kufahamu kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, haiwashinikiza marafiki na waungaji wake mkono, bali inaheshimu matakwa yao sambamba na kusisitizia udharura wa kuchaguliwa rais wa taifa la Lebanon haraka iwezekanavyo." Mwisho wa kunukuu.

 

http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/40796-uchaguzi-wa-urais-syria,-ni-tangazo-la-kufeli-njama-za-maadui

Read More 0 Comments

Mon

26

May

2014

Nasrullah: Hizbullah ilivuruga mipango ya Wamagharibi

13- Kiswahili

Sayyid Hassan Nasrullah  Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah nchini Lebanon, amesema kuwa, idi ya muqawama na kukombolewa kusini mwa Lebanon ni idi ya taifa na umma mzima wa Kiislamu. Sayyid Hassan Nasrullah aliyasema hayo jana jioni katika hotuba aliyoitoa katika sherehe za kuadhimisha miaka 14 ya ushindi wa muqawama dhidi ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na kuondoka utawala huo katika maeneo ya kusini mwa nchi hiyo ya Kiarabu. Alisisitiza kuwa, ushindi huo na mwingineo wa harakati ya muqawama dhidi ya Wazayuni, umepelekea kusambaratisha mpango wa Mashariki ya Kati mpya wa Marekani na utawala huo haramu.

Aidha amefafanua zaidi kuwa, ushindi huo ni ushindi wa Lebanon, Waarabu na umma mzima wa Kiislamu na kwamba hakuna kundi lolote linaloweza kujisifu kwamba ushindi huo ni wake pekee. Amesema, ni lazima kujiweka tayari kukabiliana na adui na kwamba muqawama hivi sasa ndio njia pekee ya kiulinzi kwa ajili ya tataifa hilo. Kwa upande mwingine Katibu Mkuu wa harakati ya muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa, ili uweze kufikia mafanikio yake katika kuwalinda wananchi, taifa na serikali ya Lebanon, muqawa unahitajia msaada wa kirafiki wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Syria hasa kwa kuzingatia kuwa, adui Mzayuni amejizatiti vilivyo.

http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/40510-nasrullah-hizbullah-ilivuruga-mipango-ya-israel-na-marekani

Read More 1 Comments

Sun

30

Mar

2014

Nasrullah: Hizbullah imeiokoa Lebanon

13- Kiswahili

Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa, kama wanamapambano wa harakati hiyo wasingeliingia nchini Syria, makundi ya kigaidi na kitakfiri yangeliwanyanyasa wananchi wote wa Lebanon.

Akizungumza kwa njia ya televisheni hapo jana, Sayyid Hassan Nasrullah amesisitiza kuwa, kama makundi ya kitakfiri na kigaidi yangelipata ushindi nchini Syria, asingelibakia mtu au harakati yoyote nchini Lebanon.

Nasrullah ameongeza kuwa wanamapambano wa Hizbullah waliingia nchini Syria yapata mwaka mmoja na nusu uliopita, wakati ambao makundi ya kigaidi yalikuwa yamebakisha mita 200 tu kulifikia kaburi la Bibi Zainab bint Ali (as) mjukuu wa Mtume Mtukufu Muhammad SAW.

Katibu Mkuu wa Hizbullah amesisitiza kuwa, kaburi la Bibi Zainab (as) linaheshimiwa na Waislamu wote wa Madhehebu ya Kishia na Kisuni duniani.

Sayyid Hassan Nasrullah ameongeza kuwa, wakati vilipoanza vita vya Syria, Hizbullah ilipendekeza kutatuliwa mgogoro wa nchi hiyo  kwa njia za kisiasa, lakini harakati hiyo ilibadilisha msimamo huo baada ya kuziona nchi wanachama wa  Jumuiya ya Nchi za Kiarabu zikifadhilisha njia za kijeshi kuliko za kisiasa.

http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/39178-nasrullah-wanamgambo-wa-hizbullah-syria,-wameiokoa-lebanon

Read More 1 Comments

Tue

18

Feb

2014

Israel ni hatari kwa nchi za Kiislamu

19- Kiswahili

Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa harakati ya muqawama wa Kiislamu ya Lebanon Hizbullah, amekosoa kughafilika kwa nchi za Kiislamu juu ya hatari ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ambao ni tishio kwa Lebanon, palestina na ulimwengu mzima.

Sayyid Hassan amesema kuwa, hii leo nchi zote za Kiislamu zinajishughulisha na mambo yao ya ndani, huku zikisahau hatari ya utawala wa Kizayuni.

Sayyid Hassan Nasrullah ameyasema hayo jana usiku katika maadhimisho ya siku ya Shahidi. Sambamba na kuwatukuza mashahidi wa muqawama, Katibu Mkuu wa Hizbullah amezungumzia hali ya nchi za Kiislamu katika eneo hivi sasa na kuitaka Marekani na utawala wa Kizayuni kupata fundisho kwa ushindi wa muqawama na kuongeza kuwa, kile wanachokitaka Washington na Tel Aviv  ni kuliondoa taifa la Palestina kutoka katika  mstari wa mapambano kwa manufaa ya Israel.

Akiashiria uwezo mkubwa wa harakati ya Hizbullah Sayyid Hassan ameuhutubu utawala wa Kizayuni kwa kusema kuwa,  lazima adui afahamu kuwa, uwezo wa Hizbullah uliokuwa ukiogopwa na utawala wa Kizayuni hapo kabla, bado upo pale pale na umezidi kuimarika zaidi. Kwa upande mwingine amezungumzia kadhia ya Syria na kusema kuwa, Saudi Arabia imepigana kwa nguvu zake zote kutaka kuiangusha serikali ya Damascus, lakini  hii leo viongozi wa Riyadh wenyewe wamefahamu kuwa, watakuwa katika hali ngumu baada ya wapiganaji wa Kiwahabi kurejea nchini humo.

http://kiswahili.irib.ir/habari/palestina/item/38234-nasrullah-israel-ni-hatari-kwa-mchi-za-kiislamu

Read More 0 Comments

Sat

21

Dec

2013

Israel ilimuua Kamanda wa Hizbullah

14Kiswahili

Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama wa Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel ulihusika moja kwa moja kumuua shahidi Hassan al Lakkis mmoja wa makamanda wa ngazi za juu wa Hizbullah hivi karibuni. Akizungumza kwa mnasaba wa kuwakumbuka mashahidi wa Hizbullah, Sayyid Hassan Nasrullah ameongeza kuwa, shahidi al Lakkis alikuwa mmoja wa makamanda shujaa waliongoza kwa mafanikio operesheni kadhaa za kijeshi za Hizbullah dhidi ya majeshi ya Israel katika miaka ya hivi karibuni. Kamanda Hassan al Lakkis aliuawa Disemba 3 mwaka huu mbele ya nyumba yake kusini mwa Beirut, baada ya kufyatuliwa risasi kadhaa. Ameongeza kuwa, chokochoko zinazoendelea kujiri ndani ya Lebanon kwa msaada wa madola ya Magharibi, zina lengo la kuutokomeza muqawama. Katibu Mkuu wa Hizbullah amesisitiza juu ya kuundwa serikali itakayokuwa na maslahi ya kitaifa, na kwamba serikali hiyo inapasa kuyashirikisha makundi yote nchini humo.

http://kiswahili.irib.ir/habari/palestina/item/36897-nasrullah-israel-ndiyo-iliyomuua-kamanda-wa-hizbullah

Read More 0 Comments

Wed

04

Dec

2013

Mshindi wa makubaliano ya nyuklia ni mataifa ya eneo

17- Kiswahili

Sayyid Hassan Nasrullah Katibu Mkuu wa chama cha Hizbullah cha Lebanon amesema kuwa mshindi mkuu wa makubaliano ya nyuklia ya Iran ni mataifa ya eneo. Nasrullah amesema kuwa bila shaka yoyote makubaliano hayo yatakuwa na matokeo muhimu sana na kwamba mshindi mkuu wa mapatano hayo ni nchi za eneo. Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema baadhi ya nchi za Kiarabu za eneo zimekuwa zichochea vita katika eneo, lakini akasema kuwa wao wanafahamu kwamba kujiri vita kumekuwa na matokeo mabaya kwa eneo hili la Mashariki ya Kati.

Sayyid Hassan Nasrullah amesema makubaliano ya nyuklia ya Iran yamepelekea kufunguliwa ukurasa mpya wa kambi kadhaa katika duru za kimataifa.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema kuwa Saudi Arabia ilihusika katika milipuko miwili ya mabomu iliyotokea nje ya ubalozi wa Iran huko Beirut mji mkuu wa Lebanon. Nasrullah amesema hana shaka yoyote kwamba shirika la ujasusi la Saudi Arabia lina mahusiano ya karibu na brigedi za Abdullah Azzam, kundi lenye mfungamano na mtandao wa al Qaida ambalo lilikiri kuhusika na milipuko nje ya ubalozi wa Iran huko Beirut.

http://kiswahili.irib.ir/habari/mchanganyiko/item/36507-mshindi-wa-makubaliano-ya-nyuklia-ni-mataifa-ya-eneo

Read More 0 Comments

Sat

16

Nov

2013

Kuna udharura wa kushikamana na muqawama

12Kiswahili

Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah amesisitizi udharura wa kushikamana na mapambano na kuongeza  kwamba hiyo ndiyo njia pekee ya kuilinda nchi hiyo. Katibu Mkuu wa Hizbullah ameyasema hayo leo katika maadhimisho ya kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein (as) mjukuu wa Mtume (saw) huko kusini mwa Lebanon. Katika hotuba yake Sayyid Hassan Nasrullah amesema kama ninavyomnukuu: "Tunatangaza leo kushikamana na muqawama kama njia pekee ya kulinda nchi na watu wetu. Kama vile vile tunavyotangaza juu ya ulazima wa kuendelea na muqawama katika kukabiliana na vitisho na udharura wa kusimama Waislamu wote duniani katika kuwatetea raia madhlumu wa Palestina." Mwisho wa kunukuu. Aidha Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza juu ya umuhimu wa mshikamano wa nchi zote za Kiarabu na Kiislamu katika kutatua matatizo yaliyopo kwa njia ya mazungumzo na hekima. Kwa upande mwingine Sayyid Hassan amewataka Waislamu wa madhehebu yote kufahamu kuwa, tatizo la makundi ya takfiri yanayowakufurisha Waislamu, ni tatizo linalowakabili Waislamu wote duniani.

http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/36065-nasrullah-kuna-udharura-wa-kushikamana-na-muqawama

Read More 0 Comments

Wed

13

Nov

2013

Yanayojiri sasa yanaifurahisha Israel

13- Kiswahili

Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah amesema kuwa hali ya vita, mapigano na ukosefu wa maelewano inayotawala sasa katika nchi za Kiarabu na Kiislamu inaifurahisha Israel.

Sayyid Nasrullah ambaye jana usiku alikuwa akihutubia hadhara kubwa ya majlisi ya maombolezo ya kukumbuka tukio chungu la kuuliwa shahidi mjukuu wa Mtume (saw), Imam Hussein (as) mjini Beirut amesema kuwa mpango wa siku zote wa Israel ni kuzigawa nchi za eneo hili kwa mujibu wa hitilafu za kidini, kimadhehebu na kikabila. Amesema kuwa baada ya matukio ya Septemba 11 mwaka 2001 huko Marekani utawala ghasibu wa Israel uliichochea Washington kuanzisha vita dhidi ya nchi za Mashariki ya Kati ikiwemo Iraq.

Katibu Mkuu wa Hizbullah amesisitiza kuwa utawala haramu wa Israel unakasirishwa mno na uwezekano wa kufikiwa makubaliano kati ya Iran na nchi za kundi la 5+1 na kwamba umetangaza kuwa utatumia nguvu zote kukwamisha jambo hilo.

Amesema ubalozi wa Marekani mjini Beirut umekuwa pango la ujasusi na kusisitiza kuwa vyombo vya mawasiliano vya Hizbullah vinaweza kuisadia serikali kukabiliana na ujasusi huo.

http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/36050-nasrullah-yanayojiri-nchi-za-kiislamu-yanaifurahisha-israe

Read More 0 Comments

Tue

29

Oct

2013

Mgogoro wa Syria utatuliwe kisiasa

14Kiswahili

Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa, mgogoro wa Syria unaweza kutatuliwa kwa njia za kisiasa na mazungumzo ya maridhiano ya pande husika.

Sayyid Hassan Nasrullah amezitaka nchi zote zifanye juhudi zaidi kwa lengo la kutatua mgogoro wa Syria kwa njia ya amani. Katibu Mkuu wa Hizbullah amebainisha kuwa mamia ya maelfu ya watu wasio na hatia wameuawa kutokana na kuendelezwa mashambulio ya makundi ya kigaidi nchini Syria na kusisitiza kuwa, walimwengu wametambua ukweli kwamba mgogoro wa nchi hiyo hauwezi kutatuliwa kwa njia za kijeshi.

Sayyid Nasrullah amesema kuwa Saudi Arabia ilichukizwa mno kuona jitihada zaidi zikifanyika kwa ajili ya kutatua mgogoro wa Syria.

http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/35680-sayyid-nasrullah-mgogoro-wa-syria-utatuliwe-kisiasa

Read More 1 Comments

Sat

17

Aug

2013

Mawahabbi walihusika na mlipuko wa Beirut

14- Kiswahili

Sayyid Hassan Nasrullah Katibu Mkuu wa harakati ya Muqawama ya Lebanon Hizbullah amesema makundi yanayowakufurisha wengine ndiyo yaliyotega bomu kwenye gari na kupelekea watu 24 kuawa huko Beirut mji mkuu wa Lebanon.

Sayyid Nasrullah amesema uchunguzi uliofanywa na Hizbullah unaonyesha kuwa makundi hayo ya ukufurishaji yamehusika katika mashambulizi makubwa ya majuzi huko Lebanon.

Katibu Mkuu wa harakati ya HIzbullah ameyasema hayo jana akiwahutubia maelfu ya wafuasi wa harakati hiyo katika kukumbuka kumalizika vita vya siku 33 kati ya harakati ya Hizbullan na utawala haramu wa Israel huko katika kijiji cha kusini cha Aita al Shaab.

http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/34066-mawahabbi-walihusika-na-mlipuko-wa-beirut

0 Comments

Sat

03

Aug

2013

Utawala wa Kizayuni wa Israel lazima uangamizwe

15- Kiswahili

Katibu Mkuu wa Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa, kutokomezwa utawala wa Kizayuni wa Israel kutakuwa na manufaa kwa wananchi wa eneo  lote la Mashariki ya Kati. Akizungumza mbele ya hadhara ya watu waliokusanyika wa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds, Sayyid Hassan Nasrullah amesisitiza kuwa, kutokomezwa kikamilifu utawala  wa Kizayuni wa Israel kutakuwa na maslahi si tu kwa Palestina, bali kwa ulimwengu mzima wa Kiislamu na Kiarabu.

Nasrullah ameelezea lengo la kuhuishwa siku ya Quds na kubainisha kuwa, ulimwengu wa Kiislamu na Kiarabu pamoja na wapenda haki kote duniani hawapaswi kuzifumbia macho haki za Wapalestina. Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema kuwa, utawala wa Israel unahatarisha eneo lote la Mashariki ya Kati na kusisitiza kuwa, kipaumbele cha kwanza kinachopasa kupewa katika eneo hili, ni kukabiliana na adui Mzayuni.

http://kiswahili.irib.ir/habari/palestina/item/33769-utawala-wa-kizayuni-wa-israel-lazima-uangamizwe

Read More 0 Comments

Thu

25

Jul

2013

Hizbullah inaungawa mkono wa watu

19- Kiswahili

Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa suala muhimu kwa harakati hiyo ni kwamba inaungwa mkono na wananchi wa Lebanon, mataifa ya Kiarabu na ulimwengu wa Kiislamu.

Sayyid Hassan Nasrullah ambaye alikuwa akijibu hatua ya Umoja wa Ulaya ya kuiweka Hizbullah katika orodha yake ya makundi ya kigaidi, alisema jana jioni katika karamu ya futari iliyotayarishwa na Hibzullah mjini Beirut kwamba, wanamapambano wa Hizbullah wamebadili kanuni za mapigano, wakabatilisha mipango ya adui na kukomboa mateka na ardhi za Lebanon zilizokuwa katika makucha ya Wazayuni na wataendelea kuwa mwiba katika jicho za Israel.

http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/33569-nasrullah-hizbullah-inaungawa-mkono-wa-watu

Read More 0 Comments

Sat

20

Jul

2013

Israel inapaswa kufikiria miji yake kwanza

15- Kiswahili

Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel  katika vita vijavyo  kwanza unapaswa  kufikia hatima ya miji ya utawala huo ghasibu  kabla ya kuishambulia Bairut, na kusisitiza kwamba Israel haina ubavu tena wa kuikalia kwa mabavu ardhi ya Lebanon. Sayyid Hassan Nasrullah amesisitiza kuwa, muqawama nchini Lebanon una mitazamo, malengo, majukumu, mikakati  na sera zilizokuwa wazi kabisa. Katibu Mkuu wa Hizbullah amesisitiza kuwa, utawala wa Israel na nchi zote zilizokuwa nyuma ya utawala huo ghasibu zinaelewa kwamba, si rahisi tena kuishambulia  kijeshi  Lebanon. Sayyid Hassan Nasrullah ameelezea sababu ya kuwa dhaifu jeshi la Lebanon na kusisitiza kuwa, Iran ilitangaza kuwa tayari kulijenga na kuliimarisha jeshi la Lebanon, lakini Marekani na baadhi ya nchi za Kiarabu zilipinga vikali kwa kuhofia kwamba jeshi la Lebanon litakuwa na nguvu zaidi katika eneo.

http://kiswahili.irib.ir/habari/palestina/item/33455-nasrullah-israel-inapaswa-kufikiria-miji-yake-kabla-ya-beirut

Read More 0 Comments

Mon

17

Jun

2013

Muqawama utaendelea nchini Lebanon

16- Kiswahili

Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah nchini Lebanon  amesema kuwa, muqawama ndio umepelekea kuhifadhiwa kujitawala  nchi ya Lebanon, na kukomesha uchu na uporaji wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Akizungumza kwa mnasaba wa kuadhimisha siku ya majeruhi wa vita na muqawama wa Kiislamu,

http://kiswahili.irib.ir/habari/mchanganyiko/item/32661-nasrullah-muqawama-utaendelea-nchini-lebanon

Read More 0 Comments

Tue

28

May

2013

Hotuba ya Nasrullah, katika sherehe za ushindi wa muqawama dhidi ya Wazayuni

23- Kiswahili

Tarehe 25 Mei inasadifiana na kumbukumbu ya ushindi wa muqawama dhidi ya Wazayuni na kukombolewa maeneo ya kusini mwa Lebanon. Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya nchini Lebanon Hizbullah Sayyid Hassan Nasrullah amehutubia kumbukumbu hizo na kugusia mambo mengi.

http://kiswahili.irib.ir/uchambuzi/item/32156-hotuba-ya-nasrullah,-katika-sherehe-za-ushindi-wa-muqawama-dhidi-ya-wazayuni

Read More 0 Comments

Thu

02

May

2013

Tahadhari ya Katibu Mkuu wa Hizbullah kwa Israel

22- Kiswahili

Katika radiamali yake kuhusiana na kushtadi vitisho na uchokozi wa Israel, kukiukwa mara kwa mara ardhi ya Lebanon pamoja na harakati za kijeshi zinazozidi kwenye mpaka na nchi hiyo, Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon ameitahadharisha Israel kuhusu hatua yoyote ya kuzusha chokochoko mpya.

http://kiswahili.irib.ir/uchambuzi/item/31559-tahadhari-ya-katibu-mkuu-wa-hizbullah-kwa-israel

 

Read More 0 Comments

Thu

28

Feb

2013

Nasrullah: Waasi Syria wanashambulia vijiji vya Shia

Kiswahili
Nasrullah: Waasi Syria wanashambulia vijiji vya Shia
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebabon Sayyid Hassan Nasrullah amesema kuwa, waasi wa Syria wanaoungwa mkono na nchi za kigeni wanashambulia vijiji vya Waislamu wa madhehebu ya Shia katika mpaka wa Lebanon.
http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/30077-nasrullah-waasi-wa-syria-wanashambulia-vijiji-vya-mashia

0 Comments