Nasrullah: Hizbullah imeiokoa Lebanon

13- Kiswahili

Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa, kama wanamapambano wa harakati hiyo wasingeliingia nchini Syria, makundi ya kigaidi na kitakfiri yangeliwanyanyasa wananchi wote wa Lebanon.

Akizungumza kwa njia ya televisheni hapo jana, Sayyid Hassan Nasrullah amesisitiza kuwa, kama makundi ya kitakfiri na kigaidi yangelipata ushindi nchini Syria, asingelibakia mtu au harakati yoyote nchini Lebanon.

Nasrullah ameongeza kuwa wanamapambano wa Hizbullah waliingia nchini Syria yapata mwaka mmoja na nusu uliopita, wakati ambao makundi ya kigaidi yalikuwa yamebakisha mita 200 tu kulifikia kaburi la Bibi Zainab bint Ali (as) mjukuu wa Mtume Mtukufu Muhammad SAW.

Katibu Mkuu wa Hizbullah amesisitiza kuwa, kaburi la Bibi Zainab (as) linaheshimiwa na Waislamu wote wa Madhehebu ya Kishia na Kisuni duniani.

Sayyid Hassan Nasrullah ameongeza kuwa, wakati vilipoanza vita vya Syria, Hizbullah ilipendekeza kutatuliwa mgogoro wa nchi hiyo  kwa njia za kisiasa, lakini harakati hiyo ilibadilisha msimamo huo baada ya kuziona nchi wanachama wa  Jumuiya ya Nchi za Kiarabu zikifadhilisha njia za kijeshi kuliko za kisiasa.

http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/39178-nasrullah-wanamgambo-wa-hizbullah-syria,-wameiokoa-lebanon

Write a comment

Comments: 1
  • #1

    peter ramadhani (Thursday, 26 January 2017 03:02)

    Congraturation to sayyed nasullah,may allah protect you in east n' west over all enemies who find you around the corner