Israel ilimuua Kamanda wa Hizbullah

14Kiswahili

Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama wa Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel ulihusika moja kwa moja kumuua shahidi Hassan al Lakkis mmoja wa makamanda wa ngazi za juu wa Hizbullah hivi karibuni. Akizungumza kwa mnasaba wa kuwakumbuka mashahidi wa Hizbullah, Sayyid Hassan Nasrullah ameongeza kuwa, shahidi al Lakkis alikuwa mmoja wa makamanda shujaa waliongoza kwa mafanikio operesheni kadhaa za kijeshi za Hizbullah dhidi ya majeshi ya Israel katika miaka ya hivi karibuni. Kamanda Hassan al Lakkis aliuawa Disemba 3 mwaka huu mbele ya nyumba yake kusini mwa Beirut, baada ya kufyatuliwa risasi kadhaa. Ameongeza kuwa, chokochoko zinazoendelea kujiri ndani ya Lebanon kwa msaada wa madola ya Magharibi, zina lengo la kuutokomeza muqawama. Katibu Mkuu wa Hizbullah amesisitiza juu ya kuundwa serikali itakayokuwa na maslahi ya kitaifa, na kwamba serikali hiyo inapasa kuyashirikisha makundi yote nchini humo.

http://kiswahili.irib.ir/habari/palestina/item/36897-nasrullah-israel-ndiyo-iliyomuua-kamanda-wa-hizbullah

Write a comment

Comments: 0