Mshindi wa makubaliano ya nyuklia ni mataifa ya eneo

17- Kiswahili

Sayyid Hassan Nasrullah Katibu Mkuu wa chama cha Hizbullah cha Lebanon amesema kuwa mshindi mkuu wa makubaliano ya nyuklia ya Iran ni mataifa ya eneo. Nasrullah amesema kuwa bila shaka yoyote makubaliano hayo yatakuwa na matokeo muhimu sana na kwamba mshindi mkuu wa mapatano hayo ni nchi za eneo. Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema baadhi ya nchi za Kiarabu za eneo zimekuwa zichochea vita katika eneo, lakini akasema kuwa wao wanafahamu kwamba kujiri vita kumekuwa na matokeo mabaya kwa eneo hili la Mashariki ya Kati.

Sayyid Hassan Nasrullah amesema makubaliano ya nyuklia ya Iran yamepelekea kufunguliwa ukurasa mpya wa kambi kadhaa katika duru za kimataifa.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema kuwa Saudi Arabia ilihusika katika milipuko miwili ya mabomu iliyotokea nje ya ubalozi wa Iran huko Beirut mji mkuu wa Lebanon. Nasrullah amesema hana shaka yoyote kwamba shirika la ujasusi la Saudi Arabia lina mahusiano ya karibu na brigedi za Abdullah Azzam, kundi lenye mfungamano na mtandao wa al Qaida ambalo lilikiri kuhusika na milipuko nje ya ubalozi wa Iran huko Beirut.

http://kiswahili.irib.ir/habari/mchanganyiko/item/36507-mshindi-wa-makubaliano-ya-nyuklia-ni-mataifa-ya-eneo

Write a comment

Comments: 0