Kuna udharura wa kushikamana na muqawama

12Kiswahili

Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah amesisitizi udharura wa kushikamana na mapambano na kuongeza  kwamba hiyo ndiyo njia pekee ya kuilinda nchi hiyo. Katibu Mkuu wa Hizbullah ameyasema hayo leo katika maadhimisho ya kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein (as) mjukuu wa Mtume (saw) huko kusini mwa Lebanon. Katika hotuba yake Sayyid Hassan Nasrullah amesema kama ninavyomnukuu: "Tunatangaza leo kushikamana na muqawama kama njia pekee ya kulinda nchi na watu wetu. Kama vile vile tunavyotangaza juu ya ulazima wa kuendelea na muqawama katika kukabiliana na vitisho na udharura wa kusimama Waislamu wote duniani katika kuwatetea raia madhlumu wa Palestina." Mwisho wa kunukuu. Aidha Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza juu ya umuhimu wa mshikamano wa nchi zote za Kiarabu na Kiislamu katika kutatua matatizo yaliyopo kwa njia ya mazungumzo na hekima. Kwa upande mwingine Sayyid Hassan amewataka Waislamu wa madhehebu yote kufahamu kuwa, tatizo la makundi ya takfiri yanayowakufurisha Waislamu, ni tatizo linalowakabili Waislamu wote duniani.

http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/36065-nasrullah-kuna-udharura-wa-kushikamana-na-muqawama

Write a comment

Comments: 0