Yanayojiri sasa yanaifurahisha Israel

13- Kiswahili

Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah amesema kuwa hali ya vita, mapigano na ukosefu wa maelewano inayotawala sasa katika nchi za Kiarabu na Kiislamu inaifurahisha Israel.

Sayyid Nasrullah ambaye jana usiku alikuwa akihutubia hadhara kubwa ya majlisi ya maombolezo ya kukumbuka tukio chungu la kuuliwa shahidi mjukuu wa Mtume (saw), Imam Hussein (as) mjini Beirut amesema kuwa mpango wa siku zote wa Israel ni kuzigawa nchi za eneo hili kwa mujibu wa hitilafu za kidini, kimadhehebu na kikabila. Amesema kuwa baada ya matukio ya Septemba 11 mwaka 2001 huko Marekani utawala ghasibu wa Israel uliichochea Washington kuanzisha vita dhidi ya nchi za Mashariki ya Kati ikiwemo Iraq.

Katibu Mkuu wa Hizbullah amesisitiza kuwa utawala haramu wa Israel unakasirishwa mno na uwezekano wa kufikiwa makubaliano kati ya Iran na nchi za kundi la 5+1 na kwamba umetangaza kuwa utatumia nguvu zote kukwamisha jambo hilo.

Amesema ubalozi wa Marekani mjini Beirut umekuwa pango la ujasusi na kusisitiza kuwa vyombo vya mawasiliano vya Hizbullah vinaweza kuisadia serikali kukabiliana na ujasusi huo.

http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/36050-nasrullah-yanayojiri-nchi-za-kiislamu-yanaifurahisha-israe

Write a comment

Comments: 0